Tuesday, October 27, 2015

Wasanii wang'ara kwenye siasa: Kigoma mjini ya mpa ridhaa Baba Levo

Kwa walio wengi mna mfahamu kijana ambaye ni msanii hapa Tanzania almaarufu kama Baba Levo ambaye pia ni mchekeshaji mzuri.

Huyu kijana kaukwaa udiwani huko kata ya kigoma mjini.

Kumbe Baba Levo nae yumo… Baba Levo ameshukuru sana kwa ushindi wake huku akisema kwamba japo kashinda na anakuwa Diwani Kigoma mjini kwa miaka mitano lakini muziki hatouacha na atajitahidi pia kusaidia vijana wenye vipaji Kigoma ili waweze kutambulika kwa sanaa wanazofanya

Tunamtakia kila lakheri katika ujenzi wa taifa letu kijana mwenzetu.

Big up bro!!