Showing posts with label Politics. Show all posts
Showing posts with label Politics. Show all posts

Thursday, March 31, 2016

Nchi zingine 10 zasitisha Misaada TANZANIA

Nchi 10 kati ya 14 za Umoja wa Ulaya Zatangaza kusitisha Ufadhili wao Kwa Bajeti ya Serikali ya Tanzania Kisa ni marudio ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika hivi majuzi.

Tamko hilo limetoka ikiwa ni mwendelezo wa tamko lililo tokea March 29 2016 na bodi ya shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutotoa zaidi dola 472 sawa na Trilioni 1.4 za kitanzania kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni kufanyika kwa uchaguzi Zanzibar licha ya malalamiko ya uchaguzi huo lakini pia sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania.
Shirika la utangazaji la Uingereza BBC kupitia bbcswahili.com limeandika ripoti ifuatayo 'kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi limetangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania, hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya Marekani kuondoa msaada kutokana na uchaguzi wa Zanzibar ulivyoendeshwa'
Ikumbukwe kuwa zaidi ya asilimia 10  ya bajeti ya Tanzania inategemea msaada mwaka huu wa fedha, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya ya Mhe. Dr. J. P. Magufuli

BREAKING NEWS: Wabunge watatu wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za Rushwa

Ni tetesi zilizokuwa zinashika kasi kwenye mitandao ya kijamii zikisema wabunge kadhaa wa kamati ya kudumu ya bunge ya HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA.
Wabunge hao wamefikishwa Mahakamani Kisutu Dar es salaam mchana wa March 31 2016 kwa tuhuma za rushwa, Victor Mwambalaswa wa Lupa (CCM), Kangi Lugola wa Mwibara (CCM) na Sadiq Murad wa Mvomero (CCM) na ripoti zinasema waliomba rushwa ya TZS 30 MILIONI.

Video hii hapa kutoka millardayo.com jionee mwenyewe.

Kutokana na taarifa hii pia chama cha mapinduzi kime sikitishwa na tuhuma hizi kwa wabunge wake ambapo Msemaji wa chama hicho Ndugu Christopher Ole-Sendeka   ametoa ufafanuzi kuhusu suala la rushwa na hatua zinazoendelea huku akisikitishwa na tabia ya wabunge kujihusishwa na tabia hiyo

Barua hiyo imeabatanishwa hapa chini.

Sunday, March 6, 2016

Mh. Rais atangaza uteuzi wa katibu mkuu kiongozi mpya




Leo tarehe 6.3.2016 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amemtangaza katibu mkuu kiongozi mpya kwenye serikali yake Mhandisi John Kijazi ambaye anachukua nafasi hiyo iliyokua kwa Ombeni Sefue, katibu mkuu mpya Mhandisi John Kijazi amekua akifanya kazi kama Balozi wa Tanzania India, mtazame Rais Magufuli hapa chini.



Rais J. P. Magufuli akimshukuru Balozi Ombeni Sefue kwa mchango wake na uchapoa kazi katika miezi yake mitatu ya uongozi.
Katika uteuzi huu Mh. Rais amesema Balozi Sefue atampangia kazi nyingine.

Saturday, February 20, 2016

MAGUFULI HADI NIGERIA: Jinsi Magufuli anavyoshika kasi kwenye vyombo vya habari Duniani



Vyombo mbalimbali vya habari duniani kama Magazeti mbalimbali ya Uarabuni, Australia, South Africa na nchi nyingine kadhaa yamesifia utendaji kazi wa raisi mpya wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli hadi baadhi ya nchi zimefanya maandamano kushinikiza viongozi wao kujifunza kwa rais wetu.
Video hii imetoa mjumuisho wa jinsi magufiuli anavyo fanya kazi na jinsi mambo yanavyoonekana kuwezekana Afrika kama tukipata viongozi wenye nia thabiti ya kushughulikia watu wenye shida.


Monday, January 12, 2015

SIASA HAZICHAGUI ZATAWALA HATA KWENYE MISIBA: ONA MSIBA WA FIDEL ODINGA ULIVOKUWA

Mazishi ya Fidel Odinga, mtoto wa kwanza wa Waziri Mkuu Mstaafu, Raila A. Odinga
MWAKA 2015 umeanza kwa Simanzi kubwa iliyoikumba familia ya waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Amolo Odinga baada ya taarifa ya kifo cha mtoto mkubwa wa mwanasiasa huyo mashuhuri nchini Kenya. Taarifa ya kifo cha mtoto wa odinga ilitolewa asubuhi ya Tarehe 04/01/2015.

Sunday, January 11, 2015

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI (aka SUGU) APATA AJALI

Kuna taarifa tulizozipata jioni ya leo January 10 kupitia mitandao mbalimbali, watu wametumiana picha na taarifa kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepata ajali eneo la Kitonga, Iringa.
Picha hizo zinaonyesha Mbunge huyo amesimama na watu kadhaa pembeni ya gari aina ya Land Cruiser iliyopinduka.
Taarifa ya uhakika niliyoipata kuhusu tukio

Thursday, January 8, 2015

CHENGE AMEJIUZULU

WAKATI Watanzania wakisubiri hatima ya Waziri wa Madini na Nishati Profesa Sospeter Muhongo, ambaye Rais Kikwete alisema anamuweka kiporo kutokana na kashfa ya Escrow, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mh Andrew Chenge, ametangaza rasmi kuachia nafasi hiyo.
Bunge lililopita baada ya kujadili ripoti CAG kuhusu miamala ilyofanyika kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania, lilipitisha maazimio manane ikiwemo kuwajibishwa viongozi wa Serikali na wale wa kamati za Bunge walionekana kuhusika katika kashfa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa, Chenge alitangaza kujiuzulu nafasi yake juzi baada ya kamati yake kukutana kwenye ofisi ndogo za Bunge jijijni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya shughuli za Bunge, John Joel, alipotakiwa kuthibitisha hili, alisema hayuko ofisini, hivyo hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja.

Saturday, January 3, 2015

Taarifa ya Tume ya Uchaguzi kuhusu Zoezi la BVR la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Mfano wa mashine ya mfumo wa BVR
Ndugu Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Watendaji wa Tume, Mabibi na Mabwana.
Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisheni kwa mara nyingine katika Mkutano huu. Nawashukuru kwamba, pamoja na majukumu mengi mliyo nayo, mmeweza kuupa umuhimu wa pekee mkutano wetu huu na kuhudhuria kwa wingi. Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nasema Ahsanteni na Karibuni sana.


Katika mkutano huu, Tume inalenga kutoa taarifa kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (Pilot Registration) kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) zoezi ambalo lilikamilika wiki iliyopita.

PROF. JAY NA AFANDE SELE SASA WATANGAZA MAJIMBO YA KUGOMBEA 2015


MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, anatarajia kugombea Ubunge jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro mwaka huu. 

Akizungumza na Tanzania Daima, rafiki yake wa karibu na Profesa Jay, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, alisema kwa sasa yupo Mikumi kwa ajili ya kumsaidia Profesa Jay katika maandalizi ya uchaguzi mkuu hapo mwakani.