Thursday, November 26, 2015

Makala ya Anthony Uhembe: UBAYA WA VITU RAHISI

Asante Mungu ni siku nyingine tena umetupa upendeleo wa kuendelea kufaidi neema ya pumzi yako na uzima, kwa wagonjwa wape heri na uponyaji wako Mungu mkuu!! Amen 

Leo nimeonelea nizungumze nawe juu ya vitu rahisi rahisi kwenye maisha yako na athari zake kuelekea mafanikio yako. Hebu tutafakari pamoja juu ya mambo rahisi rahisi na juu ya mambo magumu yanayohitaji kujituma sana!! Hebu jiulize aliye leta wazo la kutengeneza ndege, meli, magari, majumba makubwa, au hata nembo ya taifa letu alifanya kirahisi hadi kuja na nembo hiyo au vitu hivyo? Bila shaka halikuwa jambo rahisi au hata kiimani tuangalie Juu ya Yesu na Mtume Muhamad walifanya kirahisi ili kuwakomboa watu? Bila shaka haikuwa rahisi!! Au je ukombozi wa nchi yetu ulikuwa ni kirahisi kuuondoa utawala wa kikoloni? Bila shaka haikuwa rahisi!! Au je ilikuwa rahisi kwako kuweza kusoma hadi kufika ulipofikia na kupata vyeti? Bila shaka haikuwa rahisi! Je ni rahisi mama kubeba mimba hadi kuja kumzaa mtoto? Bila shaka si rahisi!