Thursday, November 26, 2015

Makala ya Anthony Uhembe: UBAYA WA VITU RAHISI

Asante Mungu ni siku nyingine tena umetupa upendeleo wa kuendelea kufaidi neema ya pumzi yako na uzima, kwa wagonjwa wape heri na uponyaji wako Mungu mkuu!! Amen 

Leo nimeonelea nizungumze nawe juu ya vitu rahisi rahisi kwenye maisha yako na athari zake kuelekea mafanikio yako. Hebu tutafakari pamoja juu ya mambo rahisi rahisi na juu ya mambo magumu yanayohitaji kujituma sana!! Hebu jiulize aliye leta wazo la kutengeneza ndege, meli, magari, majumba makubwa, au hata nembo ya taifa letu alifanya kirahisi hadi kuja na nembo hiyo au vitu hivyo? Bila shaka halikuwa jambo rahisi au hata kiimani tuangalie Juu ya Yesu na Mtume Muhamad walifanya kirahisi ili kuwakomboa watu? Bila shaka haikuwa rahisi!! Au je ukombozi wa nchi yetu ulikuwa ni kirahisi kuuondoa utawala wa kikoloni? Bila shaka haikuwa rahisi!! Au je ilikuwa rahisi kwako kuweza kusoma hadi kufika ulipofikia na kupata vyeti? Bila shaka haikuwa rahisi! Je ni rahisi mama kubeba mimba hadi kuja kumzaa mtoto? Bila shaka si rahisi! 
Sasa rafiki jiulize unadhani itakuwa kazi rahisi kwako kuweza kufikia mafanikio yako au la kwa waliofanikiwa machoni pako unadhani ilikuwa rahisi kufikia hapo? Oooh hapana haikuwa rahisi! Sasa mpendwa kama unadhani na kuota ya kuwa ipo siku utakuja fanikisha ndoto zako kirahisi utakuwa unajidanganya, na bila shaka kupoteza muda bure!! Tambua haitakuwa rahisi yakupasa uamke katika hilo lindi la kudhani utapata kirahisi maana hata Mungu baada ya Adam na Eva kuasi aliwaambia watakula kwa jasho lao!! Kwahiyo hata wewe utambue hivyo utakula kwa jasho lako kwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma na ufanisi mkubwa ili ufikie malengo yako!! 

Nakumbuka kuna wakati fulani niliwaambia marafiki zangu ya kuwa nataka niende nje ya Tanzania nikafanye kazi! Wengi wa marafiki hao walinicheka, wakanidhihaki, walinitisha na kunikatisha tamaa na hadi kufikia kuniambia ya kuwa eti utaenda kufa huko na ndugu zako wasione maiti yangu! Nikawauliza wangapi wanakufa kwa malaria, ajali, magonjwa mbalimbali Tanzania nao je wapo nje? Nikasema kwangu mimi sikatishwi na maneno yao na uoga wao wa kupenda vitu rahisi na kwakuwa niendako kuna watu basi nitaenda na nitatimiza ndoto zangu!! Nashukuru nilienda na nikafanya vile nilivyotaka kufanya na kutimiza ndoto zangu na hao walionibeza walianza kunibembeleza niwaunganishe na wao huko baada ya kuona matokeo ya vile nilikuwa nafanya!! Nikajifunza kitu kuwa katika maisha usipende sana vitu rahisi maana havitakuwa na matokeo chanya katika maisha yako! Unapofanya kila jambo fanya kwa ziada jenga kufanya juu ya kiwango kwa kila jambo maishani!! Hakika utayaona matunda ya jasho lako!! 

Basi kama unaamua kulima au kujiajili au kuajiliwa hakikisha unafanya kwa ziada na kwa bidii kubwa na utafanikiwa tu!! Usiogope kuuliza, usiogope kupata washauri, usiogope kujifunza zaidi, usiogope kuwekeza hata kama kwa mwanzo haupati faida! Usiogope kamwe!!! 
••••••••••••••••••• 
Anthony Uhembe 
Life Coach

3 comments:

me said...

thats true

me said...

thanks for the encouraging words

Unknown said...

its nice courage,have got a knowledge