Tuesday, February 18, 2014

Tangazo la nafasi za kazi 517 Serikalini

Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza jumla ya nafasi wazi za kazi 517 kwa ajili ya waajiri mbalimbali nchini.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amewataka waombaji wote wa fursa za ajira serikalini kuzingatia masharti ya tangazo, ikiwa ni pamoja na kuambatisha vielelezo muhimu kabla ya kutuma barua ya maombi. Aidha, amesema nafasi hizo za kazi zimewekwa katika tovuti Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz. Ambapo ali bainisha kuwa ya mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 03 Machi, 2014.

Nafasi ni za fani nyingi sana


Tafadhali bofya hapa upate nafasi zilizo tangazwa na vigezo vyake. 

No comments: