Picha ya Joseph Mwaisango iliyo postiwa na rafiki yangu Rama Msangi ikimuonyesha binti ambaye kwa kila tofali mbili anazobeba kama anavyoonekana pichani, na kuzisafirisha kwa umbali wa mita 500, hulipwa tshs 50 tu.
Analazimika kufanya hivyo ili kuwasaidia wazazi wake katika kuiendesha familia. Ndio, ni shilingi 50 tu, na jumla itategemea amemenyeka ruti ngapi kwa siku. Hapa ni Mbeya, Tanzania, katika nchi ambayo viongozi waliopewa jukumu la kuiandalia mustakabali wake, wanadai posho ya shs 300,000/ kwa siku, haiwatoshi kwa wao kukaa kwenye kiyoyozi, kwenye kiti cha kuzunguka, na akiwa kavaa suti.
Mliosoma hesabu, mnaweza kutusaidia kuwa ili binti
huyu na familia yake waione laki tatu, atatakiwa kubeba matofali mangapi.
Sitetei na wala sio shabiki wa vurugu za wananchi, lakini ninaamini kabisa
kuwa, kuna watu wamechoka kuiona nchi hii ikiwa katika amani na wangependa siku
moja kuona inakuwaje ikiwa wananchi wataamua kushika bakora na kuanza
kuwawajibisha waliopewa nafasi.
No comments:
Post a Comment