Monday, June 30, 2014

Waajiri walioshindwa kuwasilisha taarifa za Wahitimu wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu (HESLB) Kikaangoni


Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw. Robert Kibona akitoa mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma


Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini imepanga kuwachukulia hatua waajiri wote nchini kwa kushindwa kuwasilisha taarifa za wahitimu wa elimu ya juu wanaodaiwa na Bodi hiyo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw. Robert Kibona alipokuwa akitoa mada kuhusu urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Serikali ni mjini Dodoma jana.
“Mpaka sasa tumewachukulia hatua jumla ya waajiri watano ambao wameshindwa kuwasilisha taarifa za watumishi wao wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu”  alisema Bw. Robert.

Alisema, mwajiria atakayeshindwa kutoa taarifa za wahitimu wa elimu ya juu katika Bodi kwawakati atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni saba au kutumikia kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja.

Aidha, Bw. Robert alisema kuwa mpaka sasa takribani waajiriwa18 wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kurejesha mikopo hiyo.

Bw. Robert alifafanua kuwa ilikufanikisha zoezi la urejeshaji mikopo kutoka kwa wadaiwa, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatunga sheria na mifumo mbalimbali ya kuwadhibiti wadaiwa hao.
“Tunatengeneza sheria ambazo zitawazuia wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kupata hati ya kusafiria nje ya nchi au kibali cha kusafiri hadi atakapowasilia na na Bodi.”
Pia, alisema mhitimu atakayeshindwa kulipa mkopo taarifa zake zitatangazwa kwenye vyombo vya habari na kwenye taasisi za mikopo iliasipate huduma yoyote ya kifedha.

Naye, Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Dk. Veronica Nyahende amewataka wahitimu wa elimu ya juu nchini kutumia elimu waliyonayo kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa.
Alisema changamoto ya kurejesha mikopo ni kubwa kwa upande wa wahitimu wa elimu ya juu ambao hawana kazi ama hawajajiajiri.
“Changamoto iliyopo niwahitimu kushindwa kulipa mikopo hiyo kutokana na kuwa na kipato cha chini ama kukosa ajira.”
Alisema Bodi imeingia mkataba nakampuni zitakazokusanya mikopo kwa walionufaika na mikopo hiyo nakushindwa kuilipa.
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iko katika mchakato wa kuelimisha umma na watendaji wakuu Serikalini ili kuhakikisha wanawasilisha taarifa za watumishi wao wanaodaiwa mikopo hiyo.

No comments: