Sunday, June 15, 2014

AJIRA SI JANGA!

Wizara ya mambo ya ndani Idara ya uhamiaji mwezi march ilitangaza ajira 70 za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji. Nafasi hizo zilitangazwa katika magazeti na Tovuti ya Wizara na Idara ya Uhamiaji kufuatana na taratibu Serikali zinazosimamia ujazaji wa nafasi za kazi katika utumishi wa umma kwa lengo la kuiweka wazi kwa umma wa Watanzania na matokeo yake wahitimu zaidi ya 20,000 walituma maombi ya kazi hizo.
Kufuatana na wingi wa waombaji, Wizara ilifanya zoezi la mchujo wa awali ambao hatimaye ulibakiza kiasi cha maombi 10,000 yenye waombaji wenye sifa zinazohitajika.
Kutokana na uwingi wa wasailiwa wenye sifa ambao walipita kwenye mchujowa kwanza usahili huo ilibidi ufanyikie kwenye uwanja wa taifa. katika maana hiyo wasailiwa 9930 walikuwa ni wasindikizaji wa wenzao 70 wanaotarajiwa kupata ajira hizo. kuna mawswali mengi kwa serikali, Shule, Vyuo vikuu, wahitimu na wanafunzi pia

Maswali machache kati ya hayo ni;

Je, kwa ukweli huu ajira si janga?
Kama watanzania tunalitatuaje janga hili kwa mstakabali wa ustawi wetu?
Je, wahitimu wanapewa mafunzo ya kukabili janga kama hili?
Wahitim ambao wanafikiria kuajiriwa na serikali, mashirika na makampuni binafsi wafanyaje?

......................................na mengine mengi................................?



Maandalizi ya usaili katika uwanja wa taifa




Wasailiwa wakirusha turufu zao

Hiii imevunja record jamani

habari zaidi bofya hapa

No comments: