Tuesday, August 26, 2014

KUITWA KAZINI


Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 08 Julai hadi 09 Agosti, 2014 kuwa walioorodheshwa katika tangazo hili wamefaulu usaili na wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri kama ilivyoonyeshwa katika tangazo hili. Orodha hii pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye Kanzidata(Data Base) ambao walifaulu usaili lakini  hawakuwa wamepangiwa vituo vya kazi kutokana na nafasi kuwa chache hapo awali. Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vipya vya kazi katika muda ambao umeainishwa katika barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. 

Kwa Waombaji Kazi walioitwa katika Taasisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFSA) wote kwa pamoja wanatakiwa kuripoti Ofisi za Makao Makuu zilizoko Barabara ya Nyerere, (Mpingo House), tarehe 08/09/2014 Saa 2:00 Asubuhi.2 Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite  kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.

No comments: