Monday, April 14, 2014

TUTAFAKARI: Climate change and Infrastructure Planning

Madaraja mengi yamekatika nchini kwa mvua kubwa zilizo nyesha, hata Ruvu magari yamesimama. Kihonda darajani kuna daraja limebaki nusu achilia mbali lile daraja la Bagamoyo
Planning ya sasa haithitaji uzoefu, inahitaji mtu mwenye maono ya mbele.
Hali ilivyo ni kwamba yaonekana miradi yetu, hata nyumba tunazojenga,hatuzingatii kitu ambacho siku hizi wanakiita 'climate (change) clearance'. yaani tunajenga kiangazi na kudhani hali itabaki kiangazi au mafuriko yakija ni yale yale tuliyoyazoea. Climate change bado hata watoa maamuzi hawaijui/hawaamini.
Mfano kwa watu wanaoishi Morogoro maeneo karibu ya Mazimbu Geti la mazimbu (pale mwembeni) limekuwa likifurika kwa miaka kadhaa, ilikuwaje halmashauri wapitishe ujenzi usiozingatia hali ya eneo hili? au walidhani barabara ya lami ni ngumu sana, itazuia maji kupita?

Mtaa wa Dark City Mazimbu karibu na mwembe maji yakiwa yanavuka daraja
Maeneo ya Mazimbu darajani maji yakiwa yanavuka barabara
VIBAKA NAO!!
Mdau mmoja anaripoti;
Poleni watu wa Mazimbu. Kama itanyesha tena nadhani kesho mtapita Kihonda mwisho. Wenye magari, pale Dark City muwe waangalifu. Vijana wamejipanga kukwepua. Nimeshudia bodaboda ikigonga saloon kwa nyuma ilipokaribia mwisho wa maji. Abiria na mwendesha bodaboda wakiwabado wanainuka, tayari vijana walishaanza kuchomoa parts za piki piki!!! Ni saa nne asubuhi na watu tumejaa pale. Wanajitoa kama kusaidia lakini angalieni walivyojipangaunapoongea nao.

No comments: