Nchi 10 kati ya 14 za Umoja wa Ulaya Zatangaza kusitisha Ufadhili wao Kwa Bajeti ya Serikali ya Tanzania Kisa ni marudio ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika hivi majuzi.
Tamko hilo limetoka ikiwa ni mwendelezo wa tamko lililo tokea March 29 2016 na bodi ya shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutotoa zaidi dola 472 sawa na Trilioni 1.4 za kitanzania
kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni kufanyika kwa
uchaguzi Zanzibar licha ya malalamiko ya uchaguzi huo lakini pia sheria
mpya ya makosa ya mitandao Tanzania.
Shirika la utangazaji la Uingereza BBC kupitia bbcswahili.com limeandika ripoti ifuatayo 'kundi
la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi limetangaza kusitisha
ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania, hii inafuatia uamuzi wa
shirika la utoaji misaada la serikali ya Marekani kuondoa msaada
kutokana na uchaguzi wa Zanzibar ulivyoendeshwa'
Ikumbukwe kuwa zaidi ya asilimia 10 ya bajeti
ya Tanzania inategemea msaada mwaka huu wa fedha, kwa hivyo hatua hizo za
hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya ya Mhe. Dr. J. P. Magufuli