Thursday, March 31, 2016

Kilimo cha MAPAPAI Kinalipa !!!

HEBU CHUKUA KALUKUKETA YAKO, TUFANYE HESABU..!!

Eka moja ya shamba la papai inaweza kuingiza miche 1000-1200(elfu moja hadi elfu na mia mbili)-zile mbegu fupi. 
  • Tufanye umepanda miche 1,000. Mti mmoja ukiuhudumia vema unaweza kutoa matunda hadi 120 kwa msimu. 
  • Tufanye umetoa matunda 80, tu. Tunda moja kwa bei ya shamba tufanye umeuza bei ya "kutupwa" ya Tsh. 500/= (lakini papai lililoshiba linauzwa hadi Tsh. 3,000/= sokoni). Chukua 500/= mara 80 unapata 40,000/=(elfu arobaini kwa mti mmoja). 
  • Sasa chukua 40,000/= zidisha mara 1,000 unapata 40,000,000/=(milioni arobaini). 
  • Gharama za kulima papai ekari moja haizidi milioni mbili. 



Toka kupandwa hadi kuvunwa papai inachukua miezi kumi tu. Tufanye hivi: ukishavuna hii milioni 40 jibane, usiitumie, mwaka unaofuata nenda kapande tena papai ekari 20! Kama kalukuketa yako haisumbui utapata total ya Tsh. Milioni mia nane (800,000,000/=). 
Hapo nakuruhusu chukua milioni 100 zitumbue kwa raha zako(na mtu yeyote akikuhoji kwa nini unatumbua pesa nyingi namna hiyo? Mwambie Desmond kaniruhusu!), Then, milioni 200 wekeza tena shambani, halafu milioni 500 weka benki. Naishia hapa kuhusu "kukalukuketi", malizia mwenyewe uone kama utakosa milioni 890 ndani ya miaka mitano. 
Tuache hayo. Najua utaniuliza, maswali kuhusu soko, hali ya hewa, udongo, mbegu na mengine. Tafadhali hayo maswali tafuta majibu mwenyewe, (nimekuachia home work-usilete uvivu wa kutafuniwa kila kitu). Lakini ukilima mapapai ukakosa soko hapa nchini, niletee nikupelekee Comoro na Madagascar. Kama umeungana na waliokariri kwamba hela ni ngumu zama hizi za mtumbua majipu, shauri yako, maana huo sasa ni uzembe laivu! Nimemaliza!

ooohhh maisha magumu shauri yako.....!!!


3 comments:

Unknown said...

KINACHO SUMBUA NI MTAJI

Unknown said...

NIMETAMANI SANA

Unknown said...

Mim nimkurima nipo muheza nimerima papai ninamiche mianane na papai limeshaanza kuzaa sina soko kabisa namba yangu 0711970747