Thursday, March 31, 2016

Nchi zingine 10 zasitisha Misaada TANZANIA

Nchi 10 kati ya 14 za Umoja wa Ulaya Zatangaza kusitisha Ufadhili wao Kwa Bajeti ya Serikali ya Tanzania Kisa ni marudio ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika hivi majuzi.

Tamko hilo limetoka ikiwa ni mwendelezo wa tamko lililo tokea March 29 2016 na bodi ya shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutotoa zaidi dola 472 sawa na Trilioni 1.4 za kitanzania kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni kufanyika kwa uchaguzi Zanzibar licha ya malalamiko ya uchaguzi huo lakini pia sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania.
Shirika la utangazaji la Uingereza BBC kupitia bbcswahili.com limeandika ripoti ifuatayo 'kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi limetangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania, hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya Marekani kuondoa msaada kutokana na uchaguzi wa Zanzibar ulivyoendeshwa'
Ikumbukwe kuwa zaidi ya asilimia 10  ya bajeti ya Tanzania inategemea msaada mwaka huu wa fedha, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya ya Mhe. Dr. J. P. Magufuli

No comments: