Friday, April 1, 2016

MSHAHARA WA RAIS WA TANZANIA HUU HAPA

Imekuwa vigumu sana kwa viongozi wakuu wa nchi kutaja hadharani mishahara yao wanayo lipwa lwkini hili limekuwa si kasumba tena kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. DR. John Pombe Magufuli.

Rais huyu mchapakazi wa Tanzania amempigia simu mtangazaji wa kipindi cha ‪Clouds360‬ cha ‪‎CloudsTv‬, Hudson Kamoga baada ya kusikia watu wanazungumzia kuhusu mshahara wa Rais.
Rais amesema mshahara alioukuta na ambao analipwa  ni milioni 9 na laki 5 (9,500,000)   na  wala  sio milioni 30  kama  wanavyodai wapinzani. Amelazimika kuyasema hayo wakati wa uchambuzi wa magazeti kupitia Clouds360.

akizungumza katika kipindi hicho ameahidi pia kwamba akirudi kutoka likizo yupo tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake.

Ikumbukwe kwamba Gazeti  la  Nipashe toleo  la leo tar 01. April 2016 lilikuwa na habari  iliyowanukuu waheshimiwa wabunge wa upinzani Tundu Lissu  na  Zitto Kabwe wakitaka Rais Magufuli ataje Mshahara wake na aweke wazi kama anakatwa kodi ili kuondoa sintofahamu iliyopo .
 

Katika ziara zake na hotuba zake mbalimbali za hivi karibuni, Dk. Magufuli ameahidi kupunguza mishahara ya baadhi ya vigogo inayozidi shilingi milioni 15 ili mtumishi anayepata mshahara mkubwa zaidi usizidi kiasi hicho lengo lake ikiwa ni kupunguza tofauti kubwa iliyopo kati ya kima cha chini na cha juu.

No comments: