Tuesday, April 5, 2016

Unafahamu kiasi kilichokusanywa tangu Dr. JPM aingie madarakani? soma hapa


Tangu Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Magufuli ilipoingia madarakani tarehe 5 december 2015 ilianza kwa ajenda kubwa ya kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ambapo iliipangia Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ kufikia kiwango cha TRILIONI 12.363kwenye makusanyo yake kwa mwaka 2015/2016.
April 04 2016 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alitoa ripoti inayoonyesha kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha Machi 2016 kwa kukusanya TRILIONI 1.316 ambayo ni sawa na 101.0% ya lengo la kukusanya shilingi TRILIONI 1.302
Hiki ndicho kiasi kilicho kusanywa kuanzia Desemba, 2015 hadi kufikia Machi, 2016
                                     Lengo ( Milioni)         Makusanyo halisi ( Milioni) 
December  2015        1,346,690.4                 1,403,189.8
January     2016        1,059,863.9                  1,079,993.2
February    2016       1,028,379.4                  1,040,620.8
March         2016       1,302,482.3                  1,316,072.4
Jumla ya makusanyo ya mapato kwa muda wa kuanzia mwezi Julai 2015  hadi machi 2016 ni TRILIONI 9.88 ambayo ni 99% ya lengo la makusanyo ya TRILIONI 9.98 ya miezi tisa kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
HAya ni mafanikio makubwa kwa TRA na serikali ya TAnzania. Tunawapongeza sana kwa kuongeza mapato.

No comments: