Sunday, January 11, 2015

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI (aka SUGU) APATA AJALI

Kuna taarifa tulizozipata jioni ya leo January 10 kupitia mitandao mbalimbali, watu wametumiana picha na taarifa kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepata ajali eneo la Kitonga, Iringa.
Picha hizo zinaonyesha Mbunge huyo amesimama na watu kadhaa pembeni ya gari aina ya Land Cruiser iliyopinduka.
Taarifa ya uhakika niliyoipata kuhusu tukio
hilo ni kwamba Mbunge huyo amepata ajali akiwa na wenzake wanne ndani ya gari wakitoka Mbeya kuelekea Dar, ajali hiyo imetokea eneo la Kitonga, Iringa eneo ambalo lina kona kali za barabara.
Taarifa iliyoandikwa na mwandishi Francis Godwin kwenye matukiodaima.co.tz imesema hakuna mtu aliyefariki wala kupata majeraha makubwa ila Mbunge huyo ana michubuko midogo midogo, Kamanda wa Polisi Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
PICHA ZAIDI HAPA



1 comment:

Unknown said...

Hii blog ni nzuri sababu ina dili na mambo ya kijamii na kitaaluma umejitahidi endelea kutoa taarifa muimu sir # AGC/D/12/T/0043