Saturday, January 3, 2015

PROF. JAY NA AFANDE SELE SASA WATANGAZA MAJIMBO YA KUGOMBEA 2015


MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, anatarajia kugombea Ubunge jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro mwaka huu. 

Akizungumza na Tanzania Daima, rafiki yake wa karibu na Profesa Jay, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, alisema kwa sasa yupo Mikumi kwa ajili ya kumsaidia Profesa Jay katika maandalizi ya uchaguzi mkuu hapo mwakani.




Nipo na Profesa tunawapigia kampeni wenyeviti wa mitaa na vitongoji katika uchaguzi unaoendelea, kwasababu tukiamini kwamba serikali na msingi mzuri wa uongozi inabidi uanzie chini.Ina maana nyumba ambayo itakuwa na msingi mzuri ni nyumba bora zaidi. Kwahiyo tupo hapa Mikumi tukijaaliwa uzima Profesa Jay mwakani ametangaza nia ya kugombea ubunge hapa nyumbani kwao.
Tumeanza kujenga mazingira kwenye uongozi wa chini ili mwakani Profesa akute kuna misingi imara na apate ubunge wa hapa Mikumi, kwahiyo yeye atagombea Mikumi na mimi nitagombea Morogoro mjini kwetu,” alisema.




Aliongeza kuwa, Mikumi ndipo kwao kabisa na Profesa Jay ambaye anatarajia kugombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na wameamua kuingia kwenye siasa kwasababu wameshafanya sana nyimbo za kiharakati, wameshaongea mengi kupitia muziki wao lakini bahati mbaya viongozi wamekuwa na masikio magumu.

5 comments:

NEW TRENDS BLOG said...

Hiki nikipindi cha vijana!!!
Lets do it its our time!!! #DIT

Unknown said...

Siasa ni ya vijana sasa!!
Tujipange na kuchukua Majimbo.#DIT

Unknown said...

Nivizuri kwan tunataka mabadiliko katika nchi yetu#DIT

Fashion said...

Ni jambo nzuri kwani tunataka kuona uwajibikaji wao wa kazi#DIT

Anonymous said...

Yaap thats good ideas tunataka vijana wenye mawazo mapya yenye nguvu kama wao sio wazee wanaosinzia pale .......much congrants to pfof jay and his collegue!!!ndio tz tunayoitaka