Wednesday, December 31, 2014

WAVUTI: Maoni ya mdau kuhusu hotuba ya Mh. Rais kuhusiana na ESCROW

Wengi tumemshangaa Rais wetu kwa jinsi alivyokuwa amejiekeza kuwatetea wahalifu na kamwe hakuonyesha uchungu wa hasara iliyosababishwa na wezi wale! Katika nchi wanakotoka hao vibaka kosa la kukwepa kodi lingewagharimu
hata mali na kampuni kufilisiwa; lakini la kustaabisha hapa ni Mkuu wa nchi mwenyewe alipanda ulingoni kuwatetea kana kwamba naye ni mmiliki mmojawapo wa hisa katika IPTL!

Jingine lililotuacha midomo wazi ni eti na yeye kufanya uchunguzi ndani ya uchunguzi! CAG alishafanya uchunguzi, Kamati ya Bunge walifanya uchunguzi uliopitiwa, kukosolewa na kusahihishwa ilipobidi na Bunge zima; na vyote hivyo ni vyombo vya serikali hii hii; watu wanajiuliza; haviamini vyombo vilivyoaminiwa na kupewa dhamana hivi au anataka kuleta FBI? 

Tungemwelewa endapo angetwambia waliopokea fedha na aliyegawa wangekatwa, kuhojiwa na kuchunguzwa; lakini hili la kurudia uchunguzi uliokwishafanywa kwa lengo la kuwatoa hatiani watu waliothibitika kukosea ni la kushangaza na linamweka Rais wetu upande wa wahalifu!

Mwisho haiingii kabisa akilini kutuambia eti kutaifisha IPTL kutawatisha wawekezaji! Hatua hiyo ndiyo ingekuwa mujarab ili liwe fundisho kwa wawekezaji wababaishaji kama hao. Si Marekani, Ulaya na hata Asia hiyo Kampuni iliyofanya utapeli kwa miango kadhaa ingepona; licha ya kuongezewa mkataba mwingine wa miaka 20 tena hata baada ya kushindwa kabisa kutekeleza ule wa kwanza ambapo alishindwa hata kifua Megawati 50 tu za umeme!

Chanzo: wavuti.com

No comments: