Sunday, January 11, 2015

Dunia imekwisha: Wambaka mtoto hadi kufa na kumweka kwenye sinki

MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Rwanda Nzovwe jijini Mbeya , Elika Mkubwa (8), amefariki dunia baada ya kubakwa na watu wasiojulikana. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema baada ya watu hao kufanya unyama huo, waliuweka mwili wa mtoto huyo katika sinki la kuogea kwenye nyumba moja ambayo haijakamilika ujenzi wake. Pamoja na hayo, alisema upelelezi bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo. 

Akizungumza eneo la tukio, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.

Akizungumza eneo la tukio na paparazi huru, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.

"Nilipota taarifa hiyo, niliongozana na majirani tukiwa na ndugu wa marehemu na kushuhudia mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa kwenye sinki la kuogea huku sehemu zake za siri zikiwa zimeharibiwa vibaya."

Mama mlezi wa mtoto huyo, Sala Mwandobo, alisema mtoto huyo alitoweka nyumbani kwake Januari 7 mwaka huu baada ya kuaga anakwenda kufua nguo za shule eneo la chemchemi ya maji lililopo mbali kidogo na nyumbani kwake.



SOURCE: WAVUTI.COM

8 comments:

Unknown said...

teacher hiyo picha una wekaje pamoja na maneno

Unknown said...

people dont deserve to live while their doing those bad things
DIT0103 Athumani Rahim

Unknown said...

kweli mwisho wa dunia umefika...
Pumzika kwa aman
DIT Halima.M.Juma

Dbouwman13 said...

mmmh tunaelekea wapi sasa.... kama wamemfanya ivyo uyo binti sasa sijui tutafika wapi...

Unknown said...

Kweli binadam wamekua kama wanya duuu

Unknown said...

Kwel dunia imekwisha #dit

Unknown said...

dah kweli dunia imekwisha pumzika kwa amani #DIT Ibrahim Nassoro

Unknown said...

Its so sad kwakweli. ......DIT Mabruk Rahma.M.