Thursday, January 8, 2015

Nyie EWURA ni Kwanini bei ya Mafuta kwa walaji haishuki kwa kasi?

Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa. Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 45% haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta wakiwemo wenye daladala, mabasi wala taxi na kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua. Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2000 kwa Petroli na 1900 kwa dizeli, bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.
EWURA, inasemekana wamesema kuwa bei za hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu waagizaji huagiza kwa ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo la bei. Hata hivyo bei zimeanza kushuka toka mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa wananchi.
Kinachosikitisha ni kuwa, ingekuwa bei ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na sababu za kununua kwa wingi hazingetolewa kwetu na Mamlaka husika.
Ni kweli kwamba Tanzania hununua mafuta yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo. Lakini hao wasafishaji hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo ni dhahiri lazima bei za pampu zipungue.
Vile vile ni kweli kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi hawawezi kuona unafuu wa bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za kigeni na kuuzwa kwa Sarafu yetu.
Hata hivyo, kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta ni 40% wakati shilingi imeshuka kwa chini ya 10%. Katika hali ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.
Ni dhahiri mamlaka za nchi na hasa EWURA wanapaswa kuueleza umma ni kwanini bei za mafuta hazishuki kulingana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia bila kutumia visingizio visivyo sahihi. Wananchi wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo basi bei hizo zishuke na wananchi wafaidike na punguzo hilo.

13 comments:

Unknown said...

Biashara ya mafuta wanafanya wakubwa wa nchi hivyo sio rahisi kutuhurumia masikini wanaangalia maslahi yao binafsi,, tanzania bila ufisadi inawezekana?? #RAMADHANI,Masoud

Unknown said...

Thamani ya pesa yetu imeshuka kwa kiasi kikubwa hivyo ni vigumu bei ya mafuta kushuka kwa haraka sababu mafuta hununuliwa kwa pesa za kigeni.By PASCHAL,Cresent

Unknown said...

how to choose the background color of the blogger

Unknown said...

how to choose the background color of the blogger

Unknown said...

how to choose the background color of the blogger.
SWALEHE Fakii said

Unknown said...

how to choose the background color of the blogger.
SWALEHE Fakii said

Unknown said...

Ila ukweli unajulikana kuwa wanaomiliki.sheli za mafuta ni viongoz wakubwa hivyo bei uwainapungua kwao na sio kwa watumiaji ndomana bei inashuka kwa asilimia kubwa ila sio kwa wenye daradara

Unknown said...
This comment has been removed by the author.
Unknown said...

#DIT Kwel hii ndo Tanzaniaa, Tunaishi kama tunaiqiza inafahamika kua chanzo cha yote haya ni vionqozi wetu kukosa uzalendo bado kubak na uchu wa madaraka pasina kujua wananchi wanaumia kiasi qan, na bado kunawenqine wanataka wapewe nafasi wajarib nafkir inaeza kuwa kutoa nafuu kuweka afadhari kwan hata dunia ichenji vipi paka hawez taqa mayai yatakua ndo yaleyale japo mabadiliko yatakuwepo lakin tukumbuke kwamba hata kinyonqa anabadilika lakin kamwe hawez kuchutama,eee munqu ibaliki Afrika Ee munqu walaani wote wanaosababisha watanzania kuishi kama wako location wakiandaa movie AameN

Unknown said...

mafuta ni muhimili mkubwa wa shughuli za taifa letu tunawaomba hao EWURA waliangalie vizur suala la kupandisha kiholella bei za mafuta

ts mi YUSUPH JUMANNE MSUTA

Unknown said...

sidhani kwa kuwepo kwa umeme wa gesi kwenye nchi ndo utakuwa suluhisho la kukatika kwa umeme kwasababu idadi ya watu inaongezeka siku had siku na matumizi pia yanaongezeka.#DIT

Unknown said...

EWURA Tunawaamini na msituangushe katika hili, Tupunguzieni bei ya mafuta. #Frank Matandura DIT

Unknown said...

maisha ya mtanzania yatabaki palepale kwenye dhiki hakuna cha gesi wala madini rasimali za tanzania zitabaki za wachache tu .je serikali munajua juu ya panya road walipo tokea (maisha magumu ndipo walipo tokea) EWURA mafta yanashuka bei je munaangalia juu ya nauli kwa vyombo vya usafirishaji nao wameshusha bei (NAULI) DIT .