Monday, January 12, 2015

TANGAZO: Waliopangiwa vituo vya kazi kwa kada za afya 2015

NAFASI ZA AJIRA KWA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2014/2015

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwaarifu Wizara imeanza zoezi la kuwapangia vituo vya vya kazi Wataalam wa Kada za Afya kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Wataalam wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kwa waajiri wao ndani ya siku 14 tangu tarehe ya tangazo. Aidha,waajiri wanakumbushwa kuwasilisha taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhusu wataalam ambaohawajaripoti ili kuona uwezekano wa kujaza nafasi zao.

Vilevile, waajiri wanakumbushwa kukagua vyeti halisi vya kidato cha IV na VI, Vyeti vya taaluma na vyeti vya usajili (kwa wataalam wenye masharti ya usajili kwa mujibu wa miundo yao yau tumishi).

Orodha ya majina ya wataalam waliopangiwa kazi pamoja vituowalivyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya wizara www.moh.go.tz. Wizara haitatoa barua za kupangiwa vituo vya kazi kama ilivyokuwa awali.

Nawapongeza wataalam wote kwa kupata nafasi ya kutumia utaalam wenu katika kuwahudumiwa wananchi, na ninawatakia kazi njema na utumishi uliotukuka.

Imetolewa na:-
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
06 Januari, 2015

3 comments:

Unknown said...

KAZI NJEMA WAPENDWA .....BY MOHAMED ALLY RFROM DIT

Fashion said...

Tunawaomba wafike kwenye vituo vyao huduma ya afya muhimu DIT

Unknown said...

Afya njema kwa mafanikio mema, kwaiyo wafike mapema kama ilivyo pangwa tunawaitaji watu hao ili tutimize malengo yetu#DIT2014/2015MWATOVOLWA CHARLES