Mazishi ya Fidel Odinga, mtoto wa kwanza wa Waziri Mkuu Mstaafu, Raila A. Odinga |
Mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Fidel Odinga alikutwa akiwa amefariki dunia kitandani kwake asubuhi ya tarehe 04, Januari (jumapili) baada ya kurudi nyumbani kwake alfajiri akiwa anatoka kukutana na marafiki zake .
Mara ya mwisho Fidel aliripotiwa kukutana na baba yake usiku wa jumamosi kabla ya kuagana na kwenda kukutana na rafiki zake katika sehemu ambayo haijawekwa wazi na baada ya hapo alirudi nyumbani kupumzika hadi mauti yalipomkumba.
mazishi ya mtoto huyo wa kwanza wa Raila Odinga yalifanyika Jumamosi Tarehe 10 January 2015 ambapo wanasiasa walichukua fursa ya mazishi ya Fidel Odinga kuendeleza siasa za Uchaguzi Mkuu wa 2017, huku waombolezaji wakipigia kelele waombolezaji waliotoka mrengo wa Jubilee.
Ili kujua zaidi kuhusu tetesi za chanzo cha kifo hicho na shughuli ya mazishi kwa ufupi, tafadhali tizama video zilizopachikwa hapo chini...
6 comments:
R.I.P FIDEL ODINGA ,DIT, PASCHAL Cresent
siasa imechukua nafasi kubwa sana kwenye maisha ya jamiii za wana africa mashariki, sikuhizi sio misibani tu bali hata kwenye vitua vya daladala watu wanatumia fursa ya kunadi sera za vyama wanavyoviamini, nafikiri ifikie Wakati sasa wananchi tujitambue na tujifunze kubadilika kuendana na wakati!
SIASA MPAKA KWENYE MISIBA TUNAKWENDA WAPI JAMANI MBONA TUNAIHARIBU JAMII HIVI....BY MOHAMED ALLY R FROM DIT2014/2015
KWELI SIASA NI MCHEZO MCHAFU YANI HADI MSIBANI, BUT R.I.P FIDEL ODINGA BY MWTOVOLWA CHARLES DIT/2014/2015.
Now a day's people are focuses to archive the profit,,where are we going for a next-generation .R.I.P
Mbije Ambele(DIT)
Post a Comment