Thursday, January 8, 2015

TPDC:Umeme wa gesi kuanza mwezi ujao

Dar es Salaam. Watanzania waliokuwa wakisubiri kwa hamu kuanza kutumia umeme utokanao na mradi wa gesi asilia wa Kinyerezi, sasa watahitajika kuvuta subira kidogo kutokana na uzalishaji wa nishati hiyo kusogezwa hadi katikati ya mwezi ujao.
Awali, maofisa wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na makandarasi wa mradi kwa nyakati tofauti, walinukuliwa kuwa ujenzi ungekamilika Desemba mwaka jana na uzalishaji wa majaribio ungeanza mapema mwezi huu.
Hata hivyo, ripoti ya maendeleo ya mradi huo iliyotolewa jana na TPDC inaonyesha kuwa baadhi ya masuala ya ujenzi na ununuzi yanatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu na Februari.
Ripoti hiyo inaonyesha
kuwa ujenzi wa mradi mzima wa bomba hilo la gesi linalotokea Mtwara hadi Kinyerezi, ulikuwa umekamilika kwa asilimia 94.8 wakati ununuzi ulikuwa ni asilimia 99 mwishoni mwa Novemba.
Akielezea kilichochelewesha, Meneja wa mradi huo kutoka TPDC, Kapuulya Musomba alisema kuwa uzalishaji wa majaribio umesogezwa kutokana na tatizo la usafirishaji wa vifaa lililoathiri ratiba ya awali. Uzalishaji rasmi unatarajiwa kuanza Juni mwaka huu.
“Kuna wakati tulikuwa tukitegemea mitambo iliyoingia bandarini ingetolewa ndani ya wiki moja, lakini haikuwa hivyo,” alisema Musomba.
Kuhusu uwapo wa uchakachuaji wa kuongeza bei mara mbili ya mradi huo, Musomba alisema kiasi cha Sh2 trilioni walizoomba kukamilisha ujenzi huo ndizo zilizomo kwenye mkataba. Novemba, 2014 akiwa mjini Nzega, mkoani Tabora, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwatuhumu vigogo wa Serikali kwa ufisadi wa kuongeza Dola 600 milioni za Marekani (Sh1.02 trilioni) katika ujenzi wa mradi huo hali iliyofanya gharama ziongezeke mara mbili na kufikia Sh2.4 trilioni.
Alisema kuwa awali kampuni inayojenga bomba hilo, ilisema gharama halisi za mradi huo ilikuwa Sh1.20 trilioni, lakini wao wakaongeza mara mbili ya fedha hizo kwa manufaa yao binafsi.

8 comments:

Unknown said...

YEAP DIT1

Unknown said...

Watanzania tumeshazoea kusikiliza ahadi na mipango miiingi kama hiyo,lakini ngoja tuone maybe yaweza kuja kuwa#JOHN CHITAPA,DIT

Rahito said...

uongozi wa tanzania ni mipango bila malengo ndio maana ahadi nyingi zinashindwa kutekelezwa kwa wakati hvyo nawashauri watanzania tuwe makini hasa katika future zetu tuwe wajasiliamali tuweze kufika mbali....." The beauty is inside Us"

DIT103 Rahim Athumani

Unknown said...

Pengine hili ndo suluhisho la kukatika kwa UMEMETanzania kwa Kigezo cha upungufu wa Maji Mtera. #Frank Matandura#

Unknown said...

tumechka ahad feki.hadanganyk mtu apa

Unknown said...

tunaamin tunachokiona.

Unknown said...

tunaamin tunachokiona.

Unknown said...

nafikiri hii inaweza kusaidia kupunguza mgao wa umeme na kukatika mara kwa mara #DIT