Tangu Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Magufuli ilipoingia madarakani tarehe 5 december 2015 ilianza kwa ajenda kubwa ya kupunguza matumizi ya serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ambapo iliipangia Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ kufikia kiwango cha TRILIONI 12.363kwenye makusanyo yake kwa mwaka 2015/2016.
April 04 2016 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alitoa ripoti inayoonyesha kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha Machi 2016 kwa kukusanya TRILIONI 1.316 ambayo ni sawa na 101.0% ya lengo la kukusanya shilingi TRILIONI 1.302.






