Waziri wa A. Mashariki Mh. Samwel Sitta |
Kamati
ya Uongozi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imempitisha Waziri wa Afrika Mashariki,
Samuel Sitta, kwa kauli moja kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la
Katiba, linaripoti gazeti la HabariLeo. Pia kamati hiyo imempitisha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu kuwa mgombea wa
nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo. Taarifa kutoka ndani ya kikao cha
kamati hiyo ya uongozi ya CCM iliyoketi jana, zimebainisha kuwa Andrew Chenge
aliyekuwa akitajwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti, amejitoa katika kinyang'anyiro
hicho kwa hiari yake.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, baada ya kanuni za Bunge kupitishwa, utaratibu wa
kuchukua fomu utatangazwa ambapo Sitta atakwenda kuchukua na atakuwa mgombea
pekee kutoka CCM.
Kitakachosubiriwa
ni kuona wagombea kutoka makundi mengine kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo
na kundi linalotarajiwa ni kutoka vyama vya siasa vya upinzani.
Sifa
ya kwanza imetajwa kuwa ni utayari wake katika kuliongoza Bunge hilo.
"Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa Mwenyekiti na mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya Watanzania wapate Katiba bora kama ndoto ya Rais wetu (Jakaya Kikwete) ilivyo," alinukuliwa Sitta akizungumzia nia yake.

Kisheria,
sifa za mtu anayepaswa kuongoza Bunge hilo ni pamoja na kuwa na
Shahada ya Sheria kutoka katika chuo kinachotambulika, pia kuwa na uzoefu wa kuendesha mijadala kama ya Bunge.
Shahada ya Sheria kutoka katika chuo kinachotambulika, pia kuwa na uzoefu wa kuendesha mijadala kama ya Bunge.
Sitta
anatajwa kuwa na sifa za kushika nafasi hiyo, ikiwemo uzoefu wa miaka mitano
wakati alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Inaelezwa kuwa katika Bunge hilo la Tisa wakati akiwa Spika, mijadala mizito ilijadiliwa lakini hakutetereka hata kidogo.
Inaelezwa kuwa katika Bunge hilo la Tisa wakati akiwa Spika, mijadala mizito ilijadiliwa lakini hakutetereka hata kidogo.
Waziri
huyo pia amekuwa akitajwa na wapambe wake kuwa anafaa kuwania nafasi ya
uenyekiti kwa sababu uadilifu wake hauna shaka.
Mbali na uadilifu na uzoefu wake katika uongozi wa Bunge aliloliita la kasi na
viwango, inadaiwa hata makundi mengine, wakiwemo wabunge wa upinzani na asasi
za kiraia, wanamkubali.
Mwenyewe
Sitta aliwahi kunukuliwa akieleza sababu ya kukubaliwa na wabunge wa upinzani
kuwa wanaamini akikalia kiti hicho, ataendesha Bunge hilo kwa misingi ya uwazi
na haki.
Sifa
ya nyingine anazotajwa nazo, ni uwezo wa kutumia busara kukabiliana na makundi
yenye maslahi mbalimbali na kuwaleta pamoja.
Baadhi
ya wajumbe wa Bunge hilo tayari wanamuona Sitta kuwa mjumbe pekee mwenye uwezo
huo, kutokana na uzoefu mdogo uliopatikana katika wiki mbili za Bunge hilo
Dodoma.
No comments:
Post a Comment