Jana waziri
Maghembe amewaita wawakilishi wa wafugaji waliomo kwenye bunge la katiba, amewaandalia
chakula cha kutosha, vinywaji vya kutosha na viburudisho vingine, huku wakipewa
bahasha za nauli baada ya vikao hivyo vya siri.
Waziri wa Elimu Shukuru Kawambwa pia, jana amewaita wawakilishi wa vyuo vya elimu ya juu walioko katika bunge la katiba na kuendelea na mchezo huo.
Mhe. Lowassa pia leo anakutana na wafugaji na wakulima walio wajumbe wa bunge la katiba kwa mfumo huohuo.
Hoja zao wanapokutana na makundi haya ni kupigia chapuo kura ya WAZI na kupinga ya siri, huku wakieleza namna CCM inavyopinga baadhi ya mapendekezo muhimu yaliyomo katika rasimu ya katiba. Walichofanya mawaziri hawa ndicho kinachofanywa na mawaziri wengine wa CCM, ni agizo la lazima ambalo hivi sasa linatumika hapa Dodoma.

CCM ni
chama kikubwa na kikongwe. Rais wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa CCM ndiye
alitangaza na kuanzisha mchakato wa katiba, mabilioni ya fedha yametumika
kukusanya maoni ya wananchi na yametumika pia kuilipa tume, kuitisha mabaraza
ya katiba na mabilioni yametumika kuitisha bunge maalum ya katiba.
Leo, CCM na
mawaziri wao wanatumia fedha na kutoa rushwa ili kupitisha matakwa yao. Masuala
haya yana ushahidi, kesho nitayasema bungeni kwa uwazi kabisa.
Tutasimamia KWELI!
Julius Mtatiro via Facebook.
Tutasimamia KWELI!
Julius Mtatiro via Facebook.
No comments:
Post a Comment