Saturday, March 15, 2014

Cheka na KITIME: Anaulizi yapi kati ya haya ulifanya ukiwa mdogo?

Wakati wa utoto wetu kuna mambo mengi huwa tunayafanya bila kujua kama yatakuwa ni historia na bila shaka kila moja anaweza kuwa alifanya walau moja kati ya haya.

-       kuchovya mkate kwenye chai
-       kuweka wali wote kwenye mchuzi
-       kuvunja mfupa ili unyonye
-       kuweka nyama pembeni na kula mwisho baada ya kumaliza chakula
-       Kuonyesha wenzio chupi mpya
-       Kuomba pipi anayokula mwenzio
-       Kulamba sahani mpaka iwe safi
-       Kuvua viatu vipya,  na kutembea navyo mkononi ili watu wavione
-       Kuvaa kaptura mbili ili ukipigwa mboko zisiume
    
Shukrani sana kwa chekanakitime.blogspot.com

No comments: