Tuesday, March 4, 2014

NYALANDU: WAFANYAKAZI WALALAMIKIA PANGUA PANGUA KATIKA WIZARA YAKO

Wiki moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kupangua wakurugenzi wizarani hupo, baadhi ya askari wa wanyamapori wameibuka na kupinga uamuzi huo, huku wakitishia kufanya mgomo.
Mmoja wa askari hao, akizungumza kwa niaba ya wenzake, alisema kwa ujumla wao wanashangazwa na jinsi Nyalandu alivyomwondoa kazini Prof Songorwa licha ya kuwa alikuwa mtendaji mzuri aliyejali wafanyakazi na kuweka uzalendo mbele.
“Aliweza kuwagundua wafanyakazi wa wizara ambao ni majangili na majina anayo kwa nini asiachwe amalize kazi yake, badala yake anafukuzwa bila kosa.” Alisema mmoja wao"
“Profesa Songorwa alikuwa Pori la Selous kufanya doria siku tatu kabla ya kuondolewa kazini, alishirikiana na askari, hatua ambayo ni nadra sana kufanywa na viongozi,” alisema mmoja wa askari hao"
Alisema endapo Rais Jakaya Kikwete hatatengua uamuzi uliofanywa na Nyalandu, watafanya mgomo ambao utasababisha tembo kuuawa.
“Huyu mtu amekaa wizarani kwa mwaka mmoja tu, amejitahidi kudhibiti matumizi mabaya ya fedha, anajituma kiasi cha kulala porini, lakini leo anaondolewa katika kazi bila sababu za kueleweka. Sisi tunahisi kuna jambo hapa,” alisema askari huyo huku akichagizwa na wenzake.
“Sisi tupo nyuma yake na hatutasita katika hilo. Kama anataka afukuze wizara nzima lakini siyo kumwondoa Songorwa.”
SOURCE: GAZETI MWANANCHI Bofya hapa


No comments: