Chuo Kikuu cha Dodoma kinawatangazia waombaji wa kazi mbalimbali kuwa usahili wa kuandika utafanyika Jumamosi ya tarehe 8 Machi, 2014 na Jumapili ya tarehe 9 Machi, 2014. Usahili huu utafanyika kuanzia saa tatu asubuhi katika kumbi za mihadhara ya Skuli ya Sanaa na Lugha kama ifuatavyo:
Jumamosi tarehe 8 Machi 2014 1. Maafisa Rasilimali Watu na Tawala 2. Maafisa Mipango 3. Madereva 4. Wahudumu 5. Makatibu Muhtasi 6. Wahudumu wa Afya Jumapili tarehe 9 Machi 2014 1. Wahasibu Wasaidizi 2. Wakaguzi wa Ndani Wasaidizi 3. Watunza Kumbumbu Wasaidizi 4. Wasimamizi wa Mifumo ya Kompyuta Mtandao 5. Wasimamizi wa Maabara Usahili wa mahojiano kwa waombaji wa kada zote za afya isipokuwa wahudumu wa afya utafanyika kuanzia Jumatatu tarehe 10 Machi, 2014. Usahili huu utafanyika kuanzia saa tatu asubuhi katika jengo la Utawala kwa utaratibu ufuatao:- Jumatatu tarehe 10 Machi 2014 1. Mafundi Wasaidizi wa Maabara 2. Mafundi Sanifu Maabara 3. Wasaidizi Kumbukumbu za Afya 4. Wahandisi Vifaa Tiba 5. Mafundi Sanifu - Dawa 6. Mafundi Afya Jumanne tarehe 11 Machi 2014 1. Wauguzi/Wakunga 2. Maafisa Uuguzi Jumatano tarehe 12 Machi 2014 - Madaktari Alhamisi tarehe 13 Machi 2014 1. Wauguzi Wahitimu 2. Madaktari Bingwa Usahili wa mahojiano kwa waombaji wa kada zote ambazo hazikuorodheshwa hapo juu utafanyika Jumatatu na Jumanne yaani tarehe 17 na 18 Machi, 2014 kama ifuatavyo: Jumatatu tarehe 17 Machi, 2014 1. Wakufunzi wa Michezo 2. Maafisa Sheria 3. Waalimu Wakufunzi 4. Maafisa Ugavi 5. Mafundi Mchundo 6. Wapokezi Wageni 7. Wahandisi Maabara Jumanne tarehe 18 Machi, 2014 1. Mafundi Sanifu 2. Maafisa Miliki Kuangalia Orodha ya wasahiliwa bofya hapa ANGALIZO: Siku ya usahili wasailiwa watatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti na vyeti halisi, vitambulisho au kadi za kupigia kura na picha moja ya pasipoti. Tarehe za usaili kwa wanataaluma zitatangazwa baadae. |
This Blog Tracks Livelihood Challenges, Possible Solutions to Problems in Societies including Innovations and Technologies
Friday, March 7, 2014
Walioitwa Kwenye Usahili Chuo Kikuu cha Dodoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
ubarikiwe kwa informaion nzuri
Post a Comment