Friday, March 28, 2014

ADHA YA USAFIRI DAR WAKATI WA MVUA KAMA SIKU YA LEO

Wakazi wa jiji la Der Es Salaam wakihangaika kwenda makazini kwa miguu kutokana na adha ya usafiri. Mvua zilizoanza kunyesha juzi usiku na kuenelea jana na leo asubuhi jijini Dar es Salaam zimesababisha adha katika makazi ya watu hasa wanaoishi katika maeneo ya mabondeni na watumiaji wa barabara kutokana na miti kuanguka na kuziba njia huku maji yakijaa barabarani na kusababisha ugumu kwa vyombo vya moto kupita, kama inavyoonekana kwenye video na picha zifuatazo.



Mitaani nako hali si shwari








                                     Mti ulioangukia barabarani na kusababisha msongamano wa magari


                                   Wakazi wa Jijini wakielekea kujitafutia riziki  za familia zao

Hii adha yote ni kutokana na miundombinu mibovu katika miji iliyo mingi tanzania. 
Je serekali inajifunza nini hapa? 
Au wanangoja watu wafe ili wakatoe rambirambi?

Tafakari ! halafu chukua hatua!!!

No comments: