Monday, March 17, 2014

ZANZIBAR: Afa Akiongea Kupitia Simu Iliyopata Hitilafu Wakati Ikichajiwa

Ali Bakari Ali (20) mkazi wa Kisima Majongoo mjini Unguja amekufa baada ya simu yake aliyokuwa akitumia ambayo ilikuwa imeunganishwa na chaja ya umeme kupata hitilafu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema Ali alikufa baada ya  kupata mshtuko wa umeme unaotokana na simu yake iliyokuwa imewekwa katika chaja ya umeme huku akifanya mawasiliano. 

“Ni kweli tumepata taarifa ya kifo cha kijana Bakari Ali ambaye alikuwa akisikiliza simu yake iliyokuwa imewekwa katika chaja ya umeme na kusababisha mshituko mkubwa,” alisema. 

Kamanda Mkadam alitoa wito kwa wananchi kuepusha ajali kama hizo kwa kuwataka kuwa waangalifu na pia kuziondoa simu zao kwenye umeme wakati wanapozisikiliza.

No comments: