Jumla ya
wagombea watano wamechukua fomu za kuwania Kiti cha Ubunge katika Jimbo la
Chalinze, Bagamoyo, zoezi ambalo litafungwa rasmi tarehe 12 Machi 2014 saa kumi
kamili alasiri, kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Uchaguzi wa Jimbo la
Bagamoyo, David Shija.
Wagombea hao ni:-
Wagombea hao ni:-
- Mathayo Torongey (CHADEMA)
- Phabian Skauki wa (CUF)
- Vuniru Hussein (NRA)
- Ramadhan Mgaya (ASP)
- Ridhiwani Kikwete (CCM)
Nayo
taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye kwenda kwa vyombo vya habari inasomeka ifuatavyo:-
Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa katika Kikao chake Maalum kilichofanyika trehe
09/03/2014 pamoja na mambo mengine:-
- Kilimteua Ndugu Ridhiwan
Kikwete kuwa Mgombea wa CCM wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Chalinze
katika Uchaguzi Mdogo utakaofanyika tarehe 06/04/2014.
- Uzinduzi wa Kampeni
utafanywa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana
na kufungwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dr. Ali Mohamed Shein.
- Kampeni zitaendeshwa na
Chama ngazi husika na kuratibiwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi, Ndugu
Nape Moses Nnauye.
Aidha,
katika kikao hicho Kamati kuu ilipokea taarifa ya maendeleo ya Kampeni za
Uchaguzi Mdogo wa JImbo la Kalenga na kuridhika na mwenezo wa Kampeni ambapo
CCM inategemea kupata ushindi mkubwa.
Chama
Cha Mapinduzi kinawatakia kampeni njema na Uchaguzi mwema wananchi wa Jimbo la
Chalinze. Vyama na Wagombea washindane kwa hoja si matusi wala kupigana.
Tuendelee kudumisha Umoja, Amani na Mshikamano wetu.
No comments:
Post a Comment