Vitu anayotakiwa apate Mama Mjamzito kila Siku ya ujauzito wake kwa Afya bora.
Mlo kamili (balanced diet), ni
muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni.
Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili
ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya
wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini;
wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini;
Nafaka na Vyakula vya
Wanga.
Vyakula hivi huupa mwili nguvu za
kufanya kazi ikiwemo ukuaji wa mtoto tumboni. Vyanzo vya wanga ni kama nafaka
mbalimbali (mahindi, mtama, ulezi, mchele, uwele n.k), viazi, ndizi, mihogo. Ni
vizuri mjamzito awe anapata nafaka kamili (whole grains) kama mahindi, ngano na
mchele usiokobolewa.
Vyakula vya Protini.
Hivi ni muhimu kwenye kuujenga
mwili, hasa kipindi cha mwezi wa 4 mpaka wa 9 ambacho viungo mbalimbali vya
mtoto vinajengwa. Ni muhimu mama apate vyakula vya protini vya kutosha ili
kuhakikisha ukuaji wa mtoto unaenda vizuri. Nyama za kuku, ng’ombe, mbuzi na
wadudu waliwao kama senene, panzi; vyanzo vya protini za mimea kama maharage,
soya, njugu, njegere, karanga, korosho n.k. Samaki, maziwa, mayai ni vyanzo
vingine vya protini muhimu. Kwa wasiotumia vyakula vya nyama, unapotumia hivyo
vyakula vya mbogamboga tumia kwa wingi kwanikiwango cha protini iliyo ndani ya
mbogamboga ni chache ukilinganisha na iliyo ndani ya vyakula vya nyama.
Vyakula vyenye protein |
Vyakula vya Mafuta.
Hutumika kwenye kuupatia mwili
nguvu pamoja na ujengaji wa seli za mwili. Mara nyingi vyakula kama nyama,
karanga, ufuta, alizeti, senene, panzi, samaki na matunda kama maparachichi
huwa na mafuta. Ni vizuri kutumia mafuta yatokanayo na mimea ili kupunguza
mafuta yenye lehemu (cholesterol) nyingi.
Mboga za Majani na Matunda.
Matunda na mboga za majani ni sehemu
muhimu sana ya mlo wakati wa ujauzito, kwani huupatia mwili vitamini, madini na
kambakamba kwa ajili ya kulainisha chakula. Vitamini husaidia kuimarisha kinga
ya mwili sambamba na ufanyaji kazi wa mwili. Madini kama ya chuma, kalsiamu,
zinki, madini joto (Iodine) na magneziamu ni muhimu kwa ukuaji salama wa mtoto
tumboni mwa mama.
Madini ya chuma
(Iron)
Mahitaji ya madini ya chuma nayo huwa makubwa kwa wajawazito.
Madini hayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu ambayo huhitajika kwa wingi na
mama pamoja na mtoto. Madini joto hupatikana kwa kula kwa wingi vyakula kama
vile nyama, samaki, mayai, vyakula vilivyopikwa kwa nafaka zisizokobolewa
(ugali wa dona, mkate mweusi, n.k) na mboga za majani kama vile spinachi na
brokoli. Ili kupata madini hayo ya kutosha kutokana na vyakula hivyo,
inashauriwa mjamzito kutumia pia vidonge vya Vitamin C (Vitamin C food
supplements).
Vitamin B9 (Folic
Acid)
Vitamini hii ni muhimu sana kwa mjamzito, ni kosa kubwa sana
la kiafya kwa mjamzito kuwa na upungufu wa vitamin hii. Vitamin B9 ndiyo
inayohusika na ukuzaji na uimarishaji wa mfumo wa fahamu wa kiumbe tumboni.
Aidha, Vitamin hii ndiyo inayotoa kinga ili viungo vya mtoto visiathirike na
kuepusha uzaaji wa watoto walemavu au wenye kasoro za viungo kama ‘midomo ya
sungura’ na kadhalika.
Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha
Vitamin B9 ni pamoja na mboga za majani, juisi ya machungwa, mapeasi, vyakula vilivyopikwa kwa ngano na mchele (hasa
brown rice) na mayai. Hata hivyo, kutokana na hali ya vyakula vyetu,
mjamzito hawezi kupata kiwango kinachotakiwa cha vitamin hiyo kwa kula vyakula
peke yake.
Ili kupata kiwango cha vitamin hiyo kinachotakiwa, mjamzito atatakiwa kutumia pamoja na vidonge vya
lishe vya Vitamin B9 ili kuepuka upungufu huo. Inashauriwa kutumia vidonge
hivyo miezi michache kabla ya kushika mimba na katika kipindi cha miezi mitatu
ya mwisho ya ujauzito, kipindi ambacho vitamin hiyo huhitajika kwa wingi.
Maji
Maji ni muhimu kwenye mmeng’enyo na
unyonywaji wa chakula, pia husaidia kuzuia choo kigumu, mwili kuvimba na
maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI). Inashauriwa mjamzito anywe maji si chini ya
lita 2.2 kwa siku, yanaweza kuwa katika chai, juisi, au maji yenyewe. Ni vema
zaidi kama akinywa maji kama maji zaidi na kupunguza vinywaji kama soda. Maji
huchangia kwa asilimia 75 ya uzito wa mtoto wako atakapozaliwa. Usipopata maji
ya kutosha utaishiwa na nguvu kwa asilimia 20 na kupata matatizo ya kukaukiwa
(dehydration) na kichwa kuuma.
Mazoezi
Mazoezi ni muhimu kwa mama mjamzito
ili kumpunguzia unene na kumfanya kuwa mwepesi wakati wa kujifungua, mama
mjamzito asipofanya mazoezi aweza kunenepa na mwisho kumletea madhara, kama
magojwa ya moyo hivyo kushindwa kujifungua vizuri. Acha fikira potofu kuwa
ukipata ujauzito lazima umchukie mtu fulani au ushindwe kula baadhi ya vitu,
ondoa hayo mawazo akilini mwako, kwasababu mimba si ugonjwa.
Pia waweza jenga akili ya mtoto
wako tangu akiwa tumboni kwa kufanya mambo mazuri ambayo ungependa mwanao aje
ayafanye atakapofika duniani. Usipendelee
kunywa soda, kahawa, chai (mfano; chai bora), kulala lala na kuwa na mawazo.
KUMBUKA; Kama unapenda kuzaa mtoto mwenye ngozi laini na inayong’aa pendelea kula karoti na matango kwa wingi.
Tazama video hii ya mwandishi wa kitabu cha RATIBA BORA YA MILO KWA MTOTO NA MAMA MJAMZITO akielezea umuhimu wa kitabu hiki.
Tazama video hii ya mwandishi wa kitabu cha RATIBA BORA YA MILO KWA MTOTO NA MAMA MJAMZITO akielezea umuhimu wa kitabu hiki.
Msikilize pia mwandishi akielezea kuhusu kitabu hiki hapa
Pata ufafanuzi zaidi kwa kusoma hapa chini
Also read more by Clicking here
1 comment:
KYOLIKE, Calvin L FST/D/2013/0026
TETE, Wanzeslaus A FST/D/2013/0003
KIMAMBO, Rachel L FST/D/2013/0058
NZIKU, Dafroza Pius FST/D/2013/0049
MWANGOSI, Lilian Caen FST/D/2013/0074
MWAFATI, Cristina I FST/D/2013/0048
MWAKILABI, Goreth C FST/D/2013/0004
LEMA, Beatrice FST/D/2013/0070
HUBI, Efraim J FST/D/2013/0012
THOMAS, Innocent M FST/E/2013/0061
MAJUMBI, Samweli P FCS/D/2013/0038
Post a Comment